Huduma 08

Suluhisho za TEHAMA na AI Automation

Tunajenga na kusimamia teknolojia inayoendesha biashara yako: tovuti na web apps zenye kasi, mifumo ya biashara iliyounganishwa, zana salama za cloud, na AI automation inayofanya kazi zinazojirudia ili watu wako wajikite kwa wateja.

Mtaalamu wa TEHAMA akikagua mifumo kwenye tablet kando ya server
08Suluhisho za TEHAMA na AI Automation

Huduma hii inafaa kwa nani?

Inafaa kwa biashara zinazokua ambazo bado zinategemea spreadsheets, karatasi au apps zisizounganishwa, timu zinazopoteza saa nyingi kwa kuingiza data na kuandaa ripoti kwa mkono, au kampuni zinazotaka mshirika mmoja wa kuaminika kwa tovuti, mifumo na TEHAMA.

Hivi ndivyo tunavyoweza kusaidia.

Njia iliyo wazi hadi utekelezaji.

Scope hubadilika kulingana na brief. Hatua za kazi hubaki rahisi.

  1. 01

    Tunakagua

    Tunaorodhesha zana mnazotumia, kazi ambazo timu inarudia na mahali ambapo muda, pesa au data vinapotea.

  2. 02

    Tunajenga

    Tunabuni na kujenga tovuti, mfumo au automation kwa hatua fupi, timu yako ikijaribu kila hatua kabla haijaanza kutumika.

  3. 03

    Tunasaidia

    Tunaifundisha timu yako, tunafuatilia tulichojenga na kuendelea kukiboresha, pamoja na msaada wa haraka panapohitajika.

Maswali kabla hujaamua.

Kama swali lako halipo hapa, liweke kwenye brief hapo chini.

Tunahitaji wataalamu wa TEHAMA kutumia mnachojenga?

Hapana. Tunabuni kwa ajili ya watu watakaoutumia kila siku, tunawafundisha na kuacha miongozo rahisi ya maandishi. Tunaendelea kupatikana kwa msaada.

Mnaweza kufanya kazi na zana tulizonazo tayari?

Mara nyingi ndiyo. Tunaunganisha zana zilizopo kama WhatsApp, mobile money, Google Workspace, Microsoft 365 na programu za uhasibu kabla ya kupendekeza kitu kipya.

Mnalindaje data yetu?

Tunatumia watoa huduma salama wa cloud, tunampa kila mtu ruhusa anayohitaji tu, tunahifadhi nakala, na tunafuata Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania. Data na akaunti zinabaki kuwa mali yako.

Tuambie biashara yako inaendeshwa na nini.

Shiriki zana mnazotumia leo na kazi mnayotaka iondoke kwa timu yako.

Hatua 1 kati ya 3 · Wewe
Tufahamiane.Tutatumia maelezo haya kukujibu tu.
Ombi lakoSuluhisho za TEHAMA na AI Automation
Mradi wako uko wapi sasa?Gusa jibu linalofaa zaidi.
Unahitaji nini zaidi? si lazima
Watu wangapi watautumia? si lazima
Bajeti ya mradi si lazima
Ungependa kuanza lini? si lazima
Mwisho: unataka nini kibadilike?Sentensi chache zinatosha.
  • Kwa kawaida tunajibu ndani ya siku moja ya kazi
  • Tunatumia taarifa zako kujibu ombi hili tu
  • Hakuna pressure ya mauzo

Unataka mazungumzo ya haraka? Ongea nasi WhatsApp ↗

Anza mradi