Taarifa ya faragha
Tuko wazi tunachokusanya. Tuko makini na unachotupa.
Imeanza kutumika: 29 Agosti 2026
Nani anasimamia taarifa
Duma Brands inasimamia rekodi za maombi yanayotumwa kupitia tovuti hii. Swali au ombi la faragha unaweza kutuma info@dumabrands.com au kupiga +255 752 911 144. Usiweke password, access key, taarifa za fedha au taarifa nyeti kwenye brief ya mradi. Tuma email kuhusu faragha.
Taarifa tunazokusanya
Ukituma fomu, tunapokea taarifa ulizoandika kama jina, biashara au taasisi, email, simu, huduma, muda, kiwango cha bajeti na brief. Pia tunaweza kurekodi fomu na ukurasa uliotumia, campaign tags, browser, mfumo wa kifaa, aina ya kifaa, lugha, timezone na makadirio ya mji, mkoa au nchi pale hosting provider anapotupa taarifa hiyo. Hatuombi GPS wala eneo lako kamili. Tunaweza kutumia alama ya siri ya IP kutambua matumizi mabaya yanayojirudia bila kuweka raw IP kwenye rekodi ya lead.
Kwa nini tunazitumia
Tunatumia taarifa hizi kukujibu, kuona kama mradi unafaa, kuandaa proposal, kupanga follow-up, kuweka kumbukumbu sahihi za mazungumzo, kuelewa njia za tovuti zinazoleta maombi na kuzuia spam. Tunazitumia kwa lengo lililoelezwa, hatua uliyotuomba, uhusiano wa kazi, wajibu wa kisheria au sababu nyingine ya biashara inayoruhusiwa. Hatuuzi taarifa za maombi wala kukuingiza kwenye promosheni isiyohusiana bila ruhusa.
Draft, lugha na mandhari
Ili brief uliyoanza isipotee unapobadili lugha, sehemu zinazofaa zinaweza kuhifadhiwa kwa muda kwenye browser tab hiyo. Draft haitumwi Duma Brands mpaka ubonyeze kutuma, na inafutwa baada ya kutumwa, baada ya saa nne au session ya tab ikiisha. Alama ya kukubali privacy notice hairudishwi yenyewe. Chaguo lako la lugha na light au dark mode linaweza kubaki kwenye local storage mpaka ufute browser data.
Providers na taarifa kuvuka mipaka
Hostinger anaendesha tovuti. Supabase anahifadhi rekodi za maombi na Resend anatuma taarifa kwa timu pamoja na confirmation email yako huduma hizo zikiwekwa. GitHub na Pages CMS zinasaidia kuchapisha website lakini hazipokei fomu kupitia public website. Duma Brands ikiweka campaign measurement, scripts za Google na Meta zitapakiwa baada tu ya kuchagua Ruhusu measurement; ukikataa hazitapakiwa. Ukichagua WhatsApp au email, provider huyo atashughulikia taarifa inayohitajika. Provider anaweza kushughulikia taarifa nje ya Tanzania chini ya taratibu na mikataba yake; tunampa kinachohitajika kwa kazi yake tu.
Muda wa kuhifadhi
Tunaweka ombi wakati linafanyiwa kazi na kwa muda unaofaa baada ya hapo ili kupanga follow-up, kuweka rekodi za biashara, kutatua mgogoro au kutimiza wajibu unaotumika. Muda hutegemea kama ombi limekuwa uhusiano wa mteja na masharti ya kisheria au kihasibu. Rekodi zisizohitajika hufutwa au kuondolewa utambulisho kwenye review za mara kwa mara. Unaweza kuomba zifutwe mapema pale sheria inaporuhusu.
Usalama
Admin access inalindwa kwa server-side authentication, password iliyohifadhiwa kama hash, secure session cookie, request verification na kuzuia majaribio mengi ya login. Database credentials hazionekani kwenye browser ya umma. Pia tunatumia access controls, encrypted connections, backups na providers wanaoaminika. Hakuna huduma ya mtandao inayoweza kuahidi usalama wa asilimia 100; tukigundua tatizo linalohitaji hatua tutalishughulikia na kutoa taarifa inapohitajika.
Haki na maamuzi yako
Unaweza kuuliza kama tuna taarifa zako, kuomba kuziona au kupata nakala, kusahihisha zisizo sahihi, kupinga au kupunguza matumizi fulani, kuondoa ruhusa uliyotoa au kuomba zifutwe inapofaa. Tunaweza kuthibitisha utambulisho wako na kubaki na taarifa chache pale sheria inapohitaji. Pia unaweza kuwasilisha suala kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Tanzania. Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Chaguo la measurement, watoto na links za nje
Hii ni tovuti ya huduma za biashara na haikulenga kukusanya taarifa za watoto. Hatufanyi uamuzi wa kisheria au wenye athari kubwa kwa kutumia mfumo wa moja kwa moja kutokana na brief. Google au Meta measurement ya hiari inabaki imezimwa mpaka uruhusu kupitia privacy choice ya website; chaguo lako linahifadhiwa kwenye browser na unaweza kuliondoa kwa kufuta site data. Measurement event hutumia ukurasa, campaign na aina ya kitendo bila kukusudia kutuma jina, email, simu au ujumbe ulioandika kwenye fomu. WhatsApp, email, ramani, vyanzo na websites nyingine zina taratibu zao za faragha.
Mabadiliko
Tunaweza kusasisha taarifa hii website, providers au masharti yanayotumika yakibadilika. Mabadiliko muhimu yataonekana hapa na tarehe ya kuanza kutumika itabadilishwa.